Kumekua na migogoro mingi ya ardhi katika maeneo tofauti hapa nchini,migogoro hii imekua ikisababishwa na watumishi wa serikali wasio waaminifu pamoja na wanunuzi na madalali wasio na uelewa wa namna gani unaweza kumiliki ardhi bila migogoro.
Maranyingi kumekuwa na watu wanauziwa ardhi ambayo inakuwa imeshauzwa Zaidi ya mara kumi,au pengine kuuziwa ardhi iliyotengwa kwamatumizi sio uliokusudia
Mambo ya kuzingatia unapotaka kununua ardhi na kuimiliki kisheria 1.Fanya utafiti kwa watu wanaozunguka eneo unalokusudia kununua
2.Fuatilia hizi taarifa kwenye manispaa au uongozi wa serikali au kwa watu wa ardhi juu ya eneo husika
3.Ukishahakiki uhalali wa umiliki wa mhusika na matumizi ya eneo husika fuata taratibu za kisheria kununua eneo husika kwa kuwahusisha wanasheria.
Kama unauza kiwanja au nyumba au unatafuta kununua kiwanja au nyumba au shamba wasiliana na mimi.






No comments:
Post a Comment